nyula blog: Tanzia

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...
Showing posts with label Tanzia. Show all posts
Showing posts with label Tanzia. Show all posts

Monday, July 4, 2016

Shelukindo Kuzikwa Alhamis Jijini Arusha .




MWILI wa Mbunge wa zamani wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), unatarajiwa kuzikwa Alhamis wiki hii.

Taarifa iliyotolewa jana na kaka wa marehemu, Enock Madimilo, ilisema taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa nyumbani kwa marehemu Dar as Salaam na Arusha.

“Tunaendelea na mipango ya mazishi hapa Arusha na nyumbani kwa marehemu, Ada Estate jijini Dar es Salaam.

“Mazishi yatafanyika hapa Arusha Alhamisi wii hii. Kwa hiyo, tunawaomba ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu, waje kumuaga mpendwa na kiongozi wao,” alisema Madimilo.

Shelukindo alifariki juzi usiku saa 2:30 akiwa nyumbani kwa mama yake mzazi, katika eneo la Olorien, jijini Arusha baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mwili wa marehemu Beatrice uliondolewa nyumbani kwa mama yake huyo alipokuwa akiuguzwa usiku huo huo na kupelekwa Hospitali ya Mount Meru.

Kutokana na msiba huo, tayari waombolezaji mbalimbali wameendelea kufika nyumbani kwa mama wa marehemu kwa ajili ya kutoa pole.

Wednesday, June 8, 2016

Magazeti ya Tanzania yameamka na hizi leo June 9, 2016.



IMG_20160609_044758
IMG_20160609_044813
IMG_20160609_044830
IMG_20160609_044846
IMG_20160609_044903
IMG_20160609_044923
IMG_20160609_044941
IMG_20160609_044958
IMG_20160609_045015
IMG_20160609_045030
Screenshot_20160609-050616 (1)
Screenshot_20160609-050606
IMG_20160609_045046
IMG_20160609_045102
IMG_20160609_045118
IMG_20160609_045135
IMG_20160609_045356
IMG_20160609_045409
IMG_20160609_045423
IMG_20160609_045437
IMG_20160609_045450
IMG_20160609_045504
IMG_20160609_045532
IMG_20160609_045546
IMG_20160609_045601
IMG_20160609_045614
IMG_20160609_045628
IMG_20160609_045642
IMG_20160609_045658
IMG_20160609_045713
IMG_20160609_045728
IMG_20160609_045743
IMG_20160609_045758
IMG_20160609_045812
IMG_20160609_045826
IMG_20160609_045839
IMG_20160609_045853
IMG_20160609_045907
IMG_20160609_045924

Wednesday, May 11, 2016

Tanzia: Msanii wa Vichekesho Mohammed Abdallah (Kinyambe) Amefariki Dunia.

Mwigizaji wa comedy Mohammed Abdallah maarufu "Kinyambe" amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya mkoa wa Mbeya alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Mungu amlaze mahali  mahali pema peponi -Amina

Tuesday, April 12, 2016

Rais Magufuli Ashiriki Ibada Ya Kumbukumbu Ya Miaka 32 Ya Kifo Cha Sokoine.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na wakristo wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Joseph Jijini Dar es salaam, kusali misa Takatifu ya kumkumbuka na kumuombea aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward  Moringe Sokine aliyefariki dunia miaka 32 iliyopita, kwa ajali ya gari katika eneo la Dakawa wakati akitokea Bungeni Dodoma.

Misa hiyo imehudhuriwa pia na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Familia ya Hayati Edward Moringe Sokoine.

Akizungumzia baada ya misa hiyo Rais Magufuli amesema anamkumbuka Hayati Edward Moringe Sokoine, kuwa alikuwa kiongozi shupavu aliyewapenda watanzania, aliyependa kuwatumikia watanzania, aliyekuwa Mchapakazi, aliyechukia rushwa, aliyechukia ufisadi na aliyechukia uonevu kwa watu wa chini.

 "Namuona ni kilelezo cha pekee katika Taifa letu la Tanzania, miaka 32 iliyopita wakati Mzee wetu Hayati Edward Moringe Sokine alipoitwa na kutangulia mbele za haki, wakati huo mimi nilikuwa JKT Mpwapwa, ninaikumbuka siku hiyo ilikuwa ya majonzi makubwa"  Amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo Rais Magufuli amesema kazi nzuri ya mtu huwa haipotei na hivyo amewasihi watanzania kuendelea kushikamana, kupendana na kuyaenzi mazuri yote yaliyofanywa na viongozi wa Taifa waliotangulia mbele za haki, wakiwemo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Hayati Abeid Amani Karume na Hayati Edward Moringe Sokoine.

Kwa upande wake Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa amemuelezea Hayati Sokoine kuwa ni Kiongozi aliyejitoa kutumikia Taifa, na kubainisha kuwa viongozi wote wanawajibika kuishi kwa mfano wake.

Rais Mstaafu Mkapa amesisitiza kuwa mfano huo wa Hayati Sokoine, ndio ulioiwezesha Tanzania kumpata kiongozi wa Sasa, Rais John Pombe Magufuli anayetaka kuonesha misingi ya uongozi bora, uadilifu, kusimamia amani, utulivu na maendeleo.

Nae Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema Hayati Sokoine hakuwa kiongozi wa kujiangalia yeye, bali Kiongozi kwa ajili ya watu, na amempongeza Rais Magufuli kwa kufuata nyayo za Hayati Sokoine katika kuliongoza Taifa.

"Kuna baadhi ya watu wanasema Rais wetu wa sasa ni sura ya Edward Moringe Sokoine" Amesema Kardinali Pengo, na kumtaka Rais Magufuli na serikali yake kusonga mbele na kujenga heshima ya nchi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
12 Aprili, 2016

Sunday, January 31, 2016

INAUMA: Majangili Waitungua Helkopta na Kumuua Rubani Capt. Roger Katika Ranchi ya Wanyapori ya Mwiba, Meatu

Watu wanaodaiwa kuwa ni majangili na wawindaji haramu wameitungua kwa risasi helkopta ya doria ya wanyamapori katika pori la akiba la maswa lililoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu kusini mwa hifadhi ya taifa ya Serengeti na kumuua rubani wa helkopita na kumjeruhi askari mmoja wa wanyamapori.

Kufuatia tukio hilo, waziri wa maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe amefika katika eneo la tukio na kusisitiza kwamba serikali kwa kushirikiana na vyombo vyote vya dola na vyombo vya ulinzi na usalama inaanzisha mkakati mpya wa kupambana na ujangili na uwindaji haramu wa maliasili ikiwemo Tembo ambao ni rasilimali muhimu kwa taifa na kwa uhifadhi wa taifa la Tanzania.

Waziri Maghembe ambae amefika kwenye eneo hilo ilipotunguliwa na kuikuta helkopita hiyo iliyokuwa inarushwa na kepten Roger Gower raia wa Uingereza ambae alifariki baada ya kujeruhiwa kwa risasi amesema tukio hilo limewakera wadau wote wa uhifadhi na serikali kwa ujumla na kamwe haliwezi kuachwa lipite bila hatua madhubuti kuchukuliwa huku akiwaonya baadhi ya watumishi wa serikali na askari wa wanyamapori wanaoshirikiana na wahalifu kuwa sasa kiama chao kimefika.

Nae kamanda wa upelelezi wa mkoa wa Simiyu Jonathan Shana amesema tukio hilo lilitokea jana jioni wakati helkopita hiyo ikiwa katika doria baada ya kusikika milio ya risasi ya majangili katika pori hilo ambapo Tembo watatu waliuwawa na kwamba watu watatu wanashikiliwa na polisi wakihojiwa kufuatia tukio hilo.

==> Hili ni tukio la kwanza  katika historia ya uhifadhi nchini mwetu kwa Majangili kumpiga  risasi na kumuua Rubani na kisha  kuangusha helikopta .

==>Kepten Roger alikuwa akienda kuongeza nguvu ya askari wa uhifadhi waliokuwa wakipambana na majangili hatari wilayani Meatu, Simiyu katika ranchi ya wanyamapori ya Mwiba.

Friday, January 29, 2016

Ubalozi India waingilia maiti kuzuiwa


Ubalozi wa India nchini umeingilia kati sakata la kuzuiwa mwili wa Mtanzania, Abel Machanga aliyekwenda kutibiwa nchini India kabla ya kufariki dunia.
Dar es Salaam. Ubalozi wa India nchini umeingilia kati sakata la kuzuiwa mwili wa Mtanzania, Abel Machanga aliyekwenda kutibiwa nchini India kabla ya kufariki dunia.
Mwili wa Machanga umezuiwa katika Hospitali ya Colombia Asia iliyopo kwenye mji wa Bangarole, hadi deni la dola 16,396 sawa na Sh 35 milioni litakapolipwa.
Ufuatiliaji huo umekuja ikiwa ni siku moja baada ya gazeti hili kuchapisha habari kuhusiana na kuzuiliwa kwa mwili huo kwa siku 27 katika Hospitali hiyo. Hivi sasa zinafikia siku 30.
Abel alifariki dunia Desemba 31 mwaka jana baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe wa kichwa aliogundulika kuwa nao baada ya kufanyiwa uchunguzi .
Julai mwaka jana, gazeti hili lilichapisha habari ya maradhi ya kijana Abel hatua iliyosaidia kupatikana kwa dola 7,700 fedha zilizohitajika kwa ajili ya matibabu yake India.
Kwa mujibu wa mmoja wa maofisa wa ubalozi, aliliambia gazeti hili kuwa taarifa hiyo imemfikia, Balozi Sandeep Arya ambaye ametaka kujua ilipo hospitali hiyo.
Balozi ameguswa na hiyo taarifa na kama inavyoonekana inaharibu picha ya India hivyo anataka kuifuatilia hiyo hospitali ingawa sijui ni kwa namna gani atalishughulikia suala hilo,” alisema.
Ofisa huyo alieleza kuwa hospitali za Colombia Asia ziko nyingi nchini India hivyo inamlazimu balozi kupata anuani kamili ya eneo ambalo Abel alipatiwa matibabu na hatimaye kuaga dunia.
Katika hatua nyingine baba wa Abel, Revocatus Machange amesema mpaka sasa amepata takribani dola 16,000 ambazo ameshazituma nchini India.
“Namshukuru Mungu wasamaria wema wamesikia kilio changu nimeshatuma kiasi kikubwa cha pesa ninachosubiri kwa sasa mwili wake utolewe hospitalii.
Kuhusu gharama za usafirishaji Machanga alisema anasubiri mwili wa Abel utolewe hospitali kisha masuala ya usafirishaji yatafuata baada ya kupimwa na kujua itagharimu kiasi gani.
Chanzo: Mwananchi

Tuesday, January 26, 2016

Maiti ya Kijana Mtanzania yazuiwa India Siku 27 SOMA HAPA


Jeneza
Mwili wa kijana, Abel Machanga (24), aliyefariki dunia Desemba 31, mwaka jana katika Hospitali ya Colombia Asia, India umekwama baada ya ndugu wa marehemu kukosa fedha za kulipa deni la Sh35 milioni wanazodaiwa na hospitali hiyo.

Takribani siku 27 zimekatika tangu kijana huyo afariki na kwa muda wote huo, baba yake; Revocatus Machanga amekuwa akihaha kuomba msaada. Abel alifariki dunia baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe wa kichwa aliogundulika kuwa nao tangu 2015 na Julai mwaka jana, gazeti hili lilichapisha habari ya maradhi yake hatua iliyosaidia kupatikana kwa dola 7,700 za Marekani zilizohitajika kwa ajili ya matibabu yake India. Mara baada ya kufika India na kufanyiwa vipimo, uongozi
wa hospitali hiyo ulitaka kuongezewa dola 5,000. “Tulijichangisha nikatuma fedha hizo matibabu yakaanza.

Novemba 30 mwaka jana, alifanyiwa upasuaji alipokuwa bado kwenye uangalizi waligundua kuwa ana degedege, bakteria karibu kila sehemu ya mwili wake na shinikizo la damu kushuka kupita kiasi,” alisema na kuongeza  wakati wakiendelea kumhudumia, waligundua maradhi mengine hivyo kudai kuongezewa dola 16,396 sawa na Sh35milioni.

“Nilikwenda Wizara ya Afya kuomba msaada, waliniahidi kuna taarifa walimuagiza mwambata wao aliyekuwa India kufuatilia.

Msemaji wa Wizara ya Afya, Nsachris Mwamaja alisema hana taarifa kuhusu suala hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi wa kina leo.

Saturday, January 23, 2016

Watu wawili wamefariki dunia na wengine,36 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la BM Morogoro.

Watu wawili wamefariki dunia na wengine 36 kujeruhiwa, kati yao wanne vibaya baàda ya basi walilokuwa wakisafiria kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea Morogoro, mali ya kampuni ya BM kuligonga ubavuni lori lililokuwa likija mbele yake na kuangukia kwenye bonde pembeni ya barabara na kupinduka mara nne, katika eneo la Lubungo Mikese, barabara  kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.
ITV imefika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na kushudia majeruhi wa basi hilo la kampuni ya BM wakiletwa kwa magari binafsi na basi jingine la kampuni hiyo, wakionekana kujeruhiwa zaidi maeneo ya kichwani, usoni na miguuni, ambapo mwandishi alilazimika kuweka kalamu pembeni na kusaidiana na wananchi wengine kuwabeba majeruhi na kuwaingiza kwa madaktari kupata huduma ya kwanza,huku vitanda vya kuwabebea vikionekana kuwa vichache ikilinganishwa na wingi wa majeruhi, ambapo baadhi ya waliohojiwa wameeleza namna ajali hiyo ilivyotokea na kulalamikia wizi uliofanywa na waliofika eneo la tukio baada ya ajali.
 
Daktari bingwa wa upasuaji katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, Francis Semwene amekiti kupokea miili ya wanaume wawili na majeruhi 36, ambapo wanne kati yao hali zao ni mbaya na wengine italazimika kuwakata baadhi ya viungo iwapo watashindikana kushonwa.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo akizungumzia ajali hiyo, amesema chanzo ni mwendo kasi na imetokea majira ya saa 3:30 usiku ikihuhusisha basi la mwisho kutoka jijini Dar es Salaam kuja Morogoro, mali ya kampuni ya BM, baada ya dereva wake kufika Lubungo eneo lenye kona na mteremko mkali, na akiwa mwendo kasi, kukutana mbele na lori likiwa na tela, likitokea uelekeo wa Morogoro kuelekea Dar es Salaam, likiwa linamalizia kupita lori jingine lililokuwa limeegesha barabarani baàda ya kuharibika, ambapo dereva wa basi aligonga tela la lori hilo lililokuwa kwenye mwendo na kukosa uelekeo na kupindukia bondeni na kusababisha vifo na majeruhi hao.