Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameungana
na wakristo wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Joseph Jijini Dar es
salaam, kusali misa Takatifu ya kumkumbuka na kumuombea aliyekuwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe
Sokine aliyefariki dunia miaka 32 iliyopita, kwa ajali ya gari katika
eneo la Dakawa wakati akitokea Bungeni Dodoma.
Misa hiyo imehudhuriwa pia na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa na Familia ya Hayati Edward Moringe Sokoine.
Akizungumzia
baada ya misa hiyo Rais Magufuli amesema anamkumbuka Hayati Edward
Moringe Sokoine, kuwa alikuwa kiongozi shupavu aliyewapenda watanzania,
aliyependa kuwatumikia watanzania, aliyekuwa Mchapakazi, aliyechukia
rushwa, aliyechukia ufisadi na aliyechukia uonevu kwa watu wa chini.
"Namuona
ni kilelezo cha pekee katika Taifa letu la Tanzania, miaka 32 iliyopita
wakati Mzee wetu Hayati Edward Moringe Sokine alipoitwa na kutangulia
mbele za haki, wakati huo mimi nilikuwa JKT Mpwapwa, ninaikumbuka siku
hiyo ilikuwa ya majonzi makubwa" Amesema Rais Magufuli.
Hata
hivyo Rais Magufuli amesema kazi nzuri ya mtu huwa haipotei na hivyo
amewasihi watanzania kuendelea kushikamana, kupendana na kuyaenzi mazuri
yote yaliyofanywa na viongozi wa Taifa waliotangulia mbele za haki,
wakiwemo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Hayati
Abeid Amani Karume na Hayati Edward Moringe Sokoine.
Kwa
upande wake Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William
Mkapa amemuelezea Hayati Sokoine kuwa ni Kiongozi aliyejitoa kutumikia
Taifa, na kubainisha kuwa viongozi wote wanawajibika kuishi kwa mfano
wake.
Rais
Mstaafu Mkapa amesisitiza kuwa mfano huo wa Hayati Sokoine, ndio
ulioiwezesha Tanzania kumpata kiongozi wa Sasa, Rais John Pombe Magufuli
anayetaka kuonesha misingi ya uongozi bora, uadilifu, kusimamia amani,
utulivu na maendeleo.
Nae
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam, Mwadhama Polycarp
Kardinali Pengo amesema Hayati Sokoine hakuwa kiongozi wa kujiangalia
yeye, bali Kiongozi kwa ajili ya watu, na amempongeza Rais Magufuli kwa
kufuata nyayo za Hayati Sokoine katika kuliongoza Taifa.
"Kuna baadhi ya watu wanasema Rais wetu wa sasa ni sura ya Edward Moringe Sokoine" Amesema Kardinali Pengo, na kumtaka Rais Magufuli na serikali yake kusonga mbele na kujenga heshima ya nchi.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
12 Aprili, 2016
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini