MWILI wa Mbunge wa zamani wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), unatarajiwa kuzikwa Alhamis wiki hii.
Taarifa
iliyotolewa jana na kaka wa marehemu, Enock Madimilo, ilisema taratibu
za mazishi zinaendelea kufanywa nyumbani kwa marehemu Dar as Salaam na
Arusha.
“Tunaendelea na mipango ya mazishi hapa Arusha na nyumbani kwa marehemu, Ada Estate jijini Dar es Salaam.
“Mazishi
yatafanyika hapa Arusha Alhamisi wii hii. Kwa hiyo, tunawaomba ndugu,
jamaa na marafiki wa marehemu, waje kumuaga mpendwa na kiongozi wao,” alisema Madimilo.
Shelukindo
alifariki juzi usiku saa 2:30 akiwa nyumbani kwa mama yake mzazi,
katika eneo la Olorien, jijini Arusha baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mwili
wa marehemu Beatrice uliondolewa nyumbani kwa mama yake huyo alipokuwa
akiuguzwa usiku huo huo na kupelekwa Hospitali ya Mount Meru.
Kutokana na msiba huo, tayari waombolezaji mbalimbali wameendelea kufika nyumbani kwa mama wa marehemu kwa ajili ya kutoa pole.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini