Yanga yawasili Uturuki na kuanza mazoezi. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Monday, June 13, 2016

Yanga yawasili Uturuki na kuanza mazoezi.




Kikosi cha Yanga kikiwa katika mazoezi viwanja vya mjini Antalya, Uturuki ambako wameweka kambi kujiandaa na mchezo dhidi ya MO Bejaia nchini Algeria.
Kikosi cha Yanga kiliondoka nchini Alfajiri ya kuamkia jana kikiwa na wachezaji 21 huku beki wa kulia Juma Abdul akiachwa kutokana na kuwa majeruhi huku Malimi Busungu, kipa Benedictor Tinocco na mshambuliaji Paul Nonga wakiwa hawapo kwenye program ya kocha Hans van der Pluijm wakati kinda Yussuf Mhilu hatakwenda kwa sababu jina lake halijasajiliwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Vincent Bossou ambaye hajarejea kutoka kwao Ivory Coast ataungana na timu ikishaelekea nchini Algeria baada ya kumaliza matatizo yake ya kifamilia kutokana na kutoiwahi kambi ya Uturuki hataiwahi.
Kiungo Salum Telela ni mchezaji pekee aliyemaliza msimu na Yanga ambaye hatasafiri, kwa sababu hajapewa Mkataba mpya baada ya kumaliza wa awali.
Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesafiri lakini hatacheza mechi hiyo ya kwanza ya Kundi A kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo uliopita dhidi ya Sagrada Esperanca nchini Angola.
Yanga itakuwa ugenini Juni 19 Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria katika mchezo wa kwanza wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia ambapo Yanga itawasili nchini humo siku mbili kabla ya mechi.
Mechi hiyo itachezeshwa na marefa wa Morocco, Bouchaib El Ahrach atakayepuliza kipyenga akisaidiwa na washika vibendera, Redouane Achik na Youssef Mabrouk.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin