Mkuu
wa mkoa wa Manyara Dr Joel Bendera amevitaka vyombo vya dola mkoani
humo kuanza kufanya uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha ya
mradi wa upimaji na uuzaji wa viwanja kwenye shamba la katani la Maisaka
lililopo mjini Babati unaowahusisha Maafisa saba wa halmashauri hiyo
akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya mji huo Bw.Omari
Mkombolwa kwa tuhuma za kumsababishia mwajiri wao hasara ya shilingi
bilioni 1.7
Akisoma taarifa hiyo mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa
huo na wilaya,wananchi na wakuu wa idara mbele ya baraza maalum la
halmashauri ya mji huo kabla ya kukabidhi taarifa ya kamati ya uchunguzi
kwa TAKUKURU, na Polisi Dr.Bendera amesema amezingatia azimio la baraza
la halmashauri hiyo la oktoba 30,2014 na kuunda kamati maalum kufuati
kuwepo kwa malalamiko mengi ya wananchi waliokosa viwanja ilhali wakiwa
wamelipia.
Hata hivyo Dr.Bendera amesema baadhi ya watuhumiwa wamehamia
halmashauri nyingine amevitaka vyombo hivyo kuwatafuta ikibidi
kuwakamata ili kuwarudisha kujibu tuhuma zakutoa zabuni kwa kampuni
zisizosajiliwa,bodi ya zabuni kupuuza kwa makusudi sheria ya
ununuzi,kugawa viwanja vingi kwa mtu mmoja,ubadhilifu na kula njama na
wakandarasi,manunuzi hewa na kughushi stakabadhi na mihuri feki
akasisitiza wakithibitika wafikishwe mahakamani.
Kwa upande mwingine Mbunge wa Jimbo la Babati Bi.Pauline Gekul
licha ya kueleza kuridhishwa na kamati hiyo kwa kuwahoji watuhumiwa hao
huku hatua inayofuata ikiwa ni kutoa nafasi kwa vyombo vya dola kufanya
uchunguzi,lakini ameomba mamlaka husika kulihoji baraza la madiwani
kwani kumekuwepo na mkanganyiko wa takwimu.
Wanaohusishwa na tuhuma hizo ni aliyekuwa Mkurugenzi wa halmashauri
hiyo Bw.Omari Mohamedi Mkombolwa, Afisa mipango Hamisi Massaka,
Mwanasheria Bw.Reginald Mtei, Mhandisi Mathias
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini