Sakata
la wafanyabishara wa darajani Zanzibar limechukua sura mpya baada ya
makamu wa pili wa rais Balozi Seif Ali Iddi amewataka wafanyabishara
wenye maduka katika jengo la darajani kuhama na serikali haitobeba
jukumu la ulipaji fidia wa aina yeyote pale zoezi la ujenzi
litakapoanza.
Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa
tamko hilo baada ya kulitembelea jengo hilo na kuangalia hatua za awali
za ujenzi ambapo amesema serikali maamuzi yake ni hayo na lazima
yafuatwe kwa vile muda wa kutosha umetolewa na pia serikali imechoka
kusifu miji ya nje na saa imepania kujenga mji wake uwe wa kisasa.
Naye waziri wa nchi afisi ya rais tawala za mikoa na idara maalum
Mhe Haji Omar Kheri amesema serikali imelazimika kuchukua hatua za
haraka za kuwahamisha wafanyabiashara hao na kukataa kuwaongezea muda
kwa vile jengo hilo ni bovu na liko hatarini kuanguka, kwa upande wake
mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mji Mkongwe Issa Sarboko amesema jengo
hilo ambalo limenjengwa 1880 litabakia katika sura na muundo huohuo kwa
vile liko katika urithi wa kimataifa duniani.
Jengo hilo la darajani maarufu kwa jina la Treni ambapo lina
wapangaji zaidi ya 60, pamoja na wafanyabiashara hao wameaza kuhama
mvutano mkubwa bado upo kwa wafanyabiashara watano ambao wanadai hawezi
kuhama kwa vile wao si wapangaji ila wamiliki wa maeneo yao na serikali
haija wahakikishia haki yao italindwa vipi na itafidiwa kwa utaratibu
upi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini