Serikali
imewataka walalamikaji wa mashauri yanayoendeshwa katika mabaraza ya
ardhi kote nchini kutoa taarifa katika mamlaka husika endapo baadhi ya
wenyeviti wanadaiwa kupindisha sheria kwa sababu ya vitendo vya rushwa
hatua inayochangia baadhi ya wananchi kuichukia serikali yao.
Akizungumza na wakazi wa mji wa Lushoto katika hafla fupi ya
uzinduzi wa baraza la ardhi litakalohudumia jimbo la Bumbuli,Lushoto na
Mlalo,Waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa William
Lukuvi amesema endapo baadhi ya wenyeviti watahisiwa kuchukua rushwa na
kuwaacha walalamikaji kuhangaikia kupata haki yao bila mafanikio
wajiondoe wenyewe kabla sheria haijachukua mkondo wake.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella amezitaka
halmashauri za wilaya zenye huduma ya mabaraza ya ardhi mkoani
humu,kusaidia mabaraza hayo kwa sababu baadhi ya mashauri yanahitaji
kwenda katika eneo linalolalamikiwa kwa ajili ya ushahidi lakini kwa
sababu serikali inakabiliwa na changamoto za ukosefu wa usafiri katika
mabaraza hayo ni vyema halmashauri ikasaidia ili kuimarisha utoaji wa
haki.
Awali wakizungumza katika uzinduzi huo,wabunge wa jimbo la Bumbuli
na Lushoto wameliomba baraza hilo kuwa mstari wa mbele katika
kuharakisha usikilizaji na utoaji wa maamuzi ya walalamikaji hasa
mashauri ya migogoro ya ardhi kwa sababu ndio changamoto kubwa
inayozorotesha maendeleo kwa wananchi wilayani humo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini