Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Azindua Mpango wa Maendeleo wa Taifa . | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Tuesday, June 7, 2016

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Azindua Mpango wa Maendeleo wa Taifa .

UCHUMI wa Tanzania unazidi kukua kwa kiwango cha asilimia 7 kwa mwaka kutokana na juhudi za makusudi zilizofanywa na Serikali ikiwemo kuimarisha miundombinu, ukuzaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano na uchimbaji wa madini.

Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wakati alipokuwa akizindua Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/2017- 2020/2021.

Majaliwa alisema Mpango huo unalenga kuboresha maisha ya Watanzania kijamii na kiuchumi ili kuwaondolea umaskini kwa kuweza mkazo katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na viwanda.

“Umaskini umepungua kwa asilimia 6.2 na bado tunaendelea kufanya juhudi kubwa ili kupunguza umaskini,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa na kuongeza kuwa watanzania 10.78 milioni bado ni maskini.

Kwa mujibu wa Majaliwa alisema kuwa ukuaji wa uchumi inabidi uwe shirikishi kwa kila mwananchi kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali.

Akizungumzia suala la uwekezaji katika viwanda, Majaliwa alisema Watanzania wanapaswa kuwezeshwa katika kupata mitaji ya kuwekeza na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na kufikia uchumi wa kati.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na  Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema wakati umefika wa kuhakikisha ukuaji wa uchumi unatiliwa mkazo na serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji hasa katika viwanda na madini.

“Tumeamua kuboresha miundombinu ikiwemo ya ujenzi wa reli, kuboresha bandari zetu na kufufua Shirika la Ndege (ATCL) na kutekeleza miradi mikubwa ya uchimbaji wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na Liganga ambavyo vitaongeza pato la mtanzania kutoka dola za Kimarekani 1006 hadi 1500 ifikapo 2020,” amesema Dkt. Mpango.

Mpango huu wa Maendeleo ambao umezinduliwa na Mhe. Waziri Mkuu una Kauli Mbiu isemayo “Kujenga Uchumi wa Viwanda ili kuchochea Mageuzi ya Uchumi na Maendeleo ya Watu”.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin