ITV imefika katika maeneo ya kata ya Lukobe manispaa ya Morogoro na
kujionea hali halisi ya maji yakiwa yamejaa huku wananchi wanaokaa
katika maeneo hayo wakieleza wasiwasi wao kutokana na kuwepo kwa
uharibifu wa mifereji inayosababishwa na watu kujenga katika mikondo ya
maji nakusababisha kukosa muelekeo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa maendeleo kata ya Lukobe
Paskali Donald amesema jitihada za ujenzi wa barabara ya Mazimbu
unatarajiwa kuanza mara moja ili kuondoa adha ya ubovu wa barabara
ambayo imekuwa ikiwakabili wananchi hao.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini