Siku
chache baada ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe
Magufuli kuzindua rasmi kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Rusumo
kilichoko kwenye mpaka wa nchi za Tanzania na Rwanda,maofisa wakuu wa
Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Mapato (TRA) wameelezea jinsi kituo
hicho kitakavyosaidia kuharakisha utendaji wa kazi na namna
kitakavyoiongezea serikali mapato.
Wakizungumza na ITV kwa nyakati tofauti maofisa hao ambao ni pamoja
na Kaimu Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli na
Kamishina mkuu wa mamlaka ya Mapato Alphayo Kidata wamesema kituo cha
huduma kwa pamoja kilichozinduliwa kitasaidia kuhakiki taarifa kwa
urahisi zaidi na kwa wakati kwa kuwa shughuli za mpakani zitafanyika
kwenye jengo moja na kitawaondolea usumbufu wasafirisha mizigo
waliokuwa wakiupata wa kukaa muda mrefu kwenye mpaka huo wakati
wakisubiri kuhakikiwa kwa mizigo waliyokuwa wakisafirisha.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini