Serikali
mkoani Pemba imewaagiza watendaji wake kuhakikisha kuwa baadhi ya
wazazi ambao watashindwa kuwahimiza watoto wao kwenda shule wakamatwe na
kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili kupunguza idadi ya vijana
kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kisiwani humo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pemba katika taarifa yake
iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya mkoani katika hafla ya
makabidhiano ya jengo la shule ya msingi Matale iliyojengwa kwa msaada
wa watu wa marekani kwa gharama ya shilingi milioni 440 kwa lengo la
kusaidia sekta ya elimu.
Kwa upande wake Afisa mdhamini elimu na mafunzo ya amani mkoani
Pemba Salim Kitwana amewataka wakazi wa Matale na vitongoji vyake
kuhakikisha kuwa wanafunzi wanasoma katika shule hiyo ya kimataifa ili
kukuza viwango vya elimu katika mkoa wa Pemba.
Kufuatia hatua wakazi wa eneo la Matale wa mkoa wa Pemba wameaswa
kulitunza jengo hilo lenye uwezo wa kuongezwa ghorofa nne kwenda juu
kulitunza ili iwe msingi bora wa kuibua vipaji vya elimu kwa watoto wa
eneo hilo .
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini