Baraza
la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani limeunda
kamati itakayochunguza tuhuma zinazowakabili wakuu wa idara tano
waliohusika katika kuvurunda na kushindwa kusimamia miradi mbalimbali ya
maendeleo ikiwemo ya umwagiliaji,ardhi na ujenzi ili kuwachukulia hatua
zinazostahiki.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya baraza hilo kujigeuza kamati ili
kuwajadili wakuu wa idara walioguswa katika tuhuma hizo ambapo
Mwenyekiti wa Halmashsuair hiyo Bw.Juma Abeid mara baada ya kikao hicho
akatoa maamuzi waliyokubaliana katika kikao chao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Bi.Martha
Mkupasi amesema kikao hicho kilikuwa cha kawaida kilicholenga kupokea
taarifa za utendaji kazi za kawaida za robo Mwaka katika idara husika
kuanzia Mwezi Oktoba hadi Desemba Mwaka jana na kukiri kuwa kikubwa
kilichojitokeza ni uzembe kwa baadhi ya wakuu wa idara katika usimamizi
na utekelezaji wa miradi mikubwa ya Maendeleo ya wananchi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini