Watu
wa jamii ya kifugaji wa kabila la Watatoga katika kijiji cha Vilima
vitatu wilaya ya Babati wamelalamikia hatua ya serikali ya mkoa wa
Manyara kupiga marufuku ukataji wa miti hata ya kujengea nyumba na
maboma kuwa umeanza kuwaathiri kwani wamekuwa wakishindwa kujenga nyumba
wanyama wakali kama Simba na Chui wanaingia kwenye makazi yao kula
mifugo pamoja na kujeruhi binadamu.
Wakizungumza na ITV iliyofika katika kijiji cha Vilima vitatu watu
kutoka jamii ya kifugaji wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakihifadhi
mazingira na wanapo taka kujenga ukata matawi madogo ya miti ili
wasiharibu mazingira na uoto wa asili lakini serikali imepiga marufuku
na sasa nyumba na maboma yamechakaa na wanyama wakali kama Simba, Chui
na Fisi wanakula wanyama na kujeruhi binadamu.
Kwa upande wao wanawake kutoka kabila la Watatoga nawo wameeleza
hali hiyo inavyo waathiri wakiwa kwenye makazi yao wakati wanaume
wanapokuwa wamesafiri na wao kubaki pekee na kushindwa kudhibiti wanyama
wanaoingia kwenye makazi yao.
ITV ilimtafuta mkuu wa wilaya ya Babati Crispine Meela ambaye
amesema serikali imefikia maamuzi ya kupiga marufuku ukataji wa miti na
utoaji wa vibali vya uvunaji wa miti ndani ya kipindi cha mwaka mmoja
baada yakuona maeneo mengi yameharibiwa vibaya yakiwemo yaliyohifadhiwa
kwa manufaa ya umma.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini