Aliyekuwa
mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif
Sharif Hamad ameamua kutumbua majipu ndani ya Serikali ya Zanzibar baada
ya kudai fedha nyingi zilitoroshwa kabla ya uchaguzi na vigogo wengi wa
SMZ wana miliki fedha nje.
Maalim Seif Sharrif Hamad ametoa kauli hio hapa Zanzibar wakati
akiongea na waandishi habari kuelezea mikakati ya Chama cha Wananchi CUF
katika kudai haki ya wananchi wa Zanzibar ambapo amesema kabla ya
uchaguzi baadhi ya viongozi walisafirisha fedha nje ya nchi na wengine
kununua majumba kwa fedha za umma ingawa hakuwataja viongozi hao.
Akizumgumzia hatua ambazo CUF imezipanga kuchukua maalim Seif
ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF amesisitiza kuwa njia kubwa itaendelea
kuwa ya amani na sio fujo wala vurugu ikiwa ni pamoja na kufuata
utaratibu wa kwenda mahakama za kimataifa ingawa zina utaratibu wake
lakini tayari baadhi ya taasisi za haki za binaadamu wameanza
kulishughulikia suala la uvunjaaji wa haki hizo.
Huu ni mkutano wa pili wa CUF kufanya kuelezea msimamo wao wa
kutoitambua Serikali ya Dk.Ali Mohamed Shein na harakati wanazozichukua
ili kuhakikisha mamauzi ya wananchi ya Ockoba mwaka jana yanaheshimiwa
na kutendeka.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini