Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limefyeka ekari tano za bangi na
kuzichoma zaidi ya tani mbili ya bangi hiyo ambayo ilikuwa imekauka na
tayari imeandaliwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda kuuzwa.
Akizungumza katika zoezi la opresheni ya ufyekaji wa bangi hiyo
iliyofanyika katika kijiji cha Mwasenase kilichopo karibu na pori la
Akiba la Maswa ,Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Simiyu,Kamshina Msaidizi wa
Polisi ,Onesmo Lyanga amesema mashamba hayo ya bangi yamepatikana
kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na kikosi cha intelijensia ambacho
kiliyagundua mashamba hayo.
Kamanda Lyanga ameonya wananchi wa kijiji hicho na vijiji vya
jirani kuendelea kulima zao hilo ambalo ni haramu na badala yake
wajikite katika kulima mazao halali ambayo yatawapatia kipato kwani
ardhi yao ni nzuri lakini badala ya kuitumia kulima mazao halali ya
mahindi na mengineo wamegeuza kilimo cha bangi kama zao halali.
Aidha katika operesheni hiyo jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata
nguo na vitu mbalimbali kama samaki ambavyo viliachwa na watu
wanaosadikiwa kuwa majangili baada ya kuona askari ambapo inasemekana
eneo hilo ndilo ambalo wamekuwa wakiandalia chakula kabla ya kuingia
hifadhini kwenda kuwinda wanyama.
Opresheni hiyo ilishirikisha askari Polisi,askari mgambo na askari
wa idara ya wanyama pori,ambapo kwa mjibu wa Kamanda Lyanga amesema
operesheni hiyo itaendelea kutokana na jeshi hilo kubaini mashamba mengi
ya bangi katika vijiji vingine.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini