Chama
cha kutetea haki za abiria nchini(CHAKUA),imeitaka serikali kuwabana
wamiliki wa magari ya abiria,pindi magari yanapopata ajali na
kusababisha majeruhi wa abiria,ili kuwagharimia matatibu na fidia.
Mwenyekiti wa chama hicho Bwana Hassan Mchanjama amesema kuwa,
kutokuwa na usimamiaji wa kuridhisha kwa vyombo hivyo,imekuwa
ukisababisha umekosaji wa haki za abiria pindi wanapopata ajali.
Bwana Mchajama amesema kuwa hali imekuwa ikisababisa malamiko mengi
kutoka kwa wahanga wa ajali wa mabasi,na hata pindi wakati wakitaka
kupewa haki zao wamekuwa wakizikosa.
Kwa upande mwingine amesema kuwa CHAKUA wamebaini kuwa kuwa watu
wengi wanaopata ajali hukosa haki zao kufuatilia kutozijua sheria za
usafiri.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini