Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) imesema itaendelea kupambana na wale wote watakaogundulika kwa wizi wa kazi za sanaa.
Agizo
hilo limetolewa na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata
alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari na kueleza kuwa wapo katika
operesheni ya kukamata wezi wa kazi za sanaa .
"Ipo
kamati ambayo inajumuisha wadau kama Bodi ya Filamu, Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA) na COSOTA ikishirikiana na Jeshi la Polisi katika
kupambana na wizi wa kazi za wasanii unaokidhiri siku hadi siku' `Alisema Kaimu Kamishna Kidata.
Serikali
ipo makini kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kukusanya mapato
hasa kuongeza maeneo ya kukusanya mapato ikiwemo eneo la kazi za sanaa
hivyo Serikali haitakubali kuona inakosa mapato hayo na yoyote anayejua
mtu au kikundi cha watu kinachofanya wizi wa kazi za sanaa atoe taarifa
ofisi za TRA.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini