Jumla
ya shilingi trilioni 1.4 imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.
Kiasi
hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi bilioni 490 kwa mwezi
ukulinganisha na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba
ambapo ,TRA ilikuwa inakusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa
mwezi.
Takwimu
hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa
habari uliolenga kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi
nchini.
Ameongeza
kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi kufikia Desemba
mwaka huo TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi trilioni 6.4 ambayo
ilikuwa ni sawa na asilimia 95.5 ya lengo la kukusanya trilioni 6.5
katika kipindi hicho.
Kaimu
Kamishna huyo ametaja sababu za kuongeza kwa makusanyo ya kodi kuwa ni
pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuweka mifumo mizuri ya
ufuatiliaji ili kumrahisishia mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila
usumbufu.
Kidata
amesema kuwa katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano ya
kuongeza mapato Mamlaka hiyo itasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato
na kuwabana wote wenye nia ya kukwepa na hatimaye kuwafikisha katika
vyombo vya sheria watakaobainika wamekwepa kodi.
Katika
hatua nyingine Kaimu Kamishina Mkuu wa TRA huyo amesema jumla ya
shillingi billioni 11.8n zimekusanywa kutoka kwa wafanyabiashara
walioondosha makasha katika Bandari Kavu kinyume na taratibu za forodha.
Amesema
kuwa makusanyo hayo yanajumuisha shilingi bilioni 5.3 kuoka kwa Kampuni
na wafanyabiashara 19 ambao wamemaliza kulipa kodi za makasha yao na
wengine 19 ambao wamelipa sehemu ya kodi ya makasha yao
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini