Makamu
wa pili wa rais wa serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali
Idd amewataka wananchi wa Zanzibar kuwa watulivu kuacha kudanganyana na
badala yake wasubiri muda utakapofika rais atakaye tangazwa ataapishwa
na kuchukua madaraka ya kuiyongoza Zanzibar.
Balozi Seif ameyasema hayo hapa Kianga Ole mara baada ya kuweka
jiwe la msingi la ujenzi wa barabara mpya kutoka Ole hadi Kengeja yenye
urefu wa kilo mita 35 ikiwa nimiongoni mwa shamrashamra ya madhimisho ya
mika 52 ya mapinduzi ya Zanzibar zinazoendelea Unguja na Pemba.
Aidha balozi Seif amesema nivyema kwa wafanyakazi kila moja kwa
nafasi yake kuwajibika kuhakikisha hawachii watu kujenga karibu na
barabara kwani sio busara kumvunjia mtu aliejenga watendaji wapo
nakumwachia kisha kumvunjia nyumba yake badala yake azuiwe wakati
anataka kujenga.
Mapema katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano na miundombino wa
serekali ya Mapinduzi Zanzibar Juma Maliki Akili amesema zaidi ya dola
milioni 12 zitatumika katika ujenzi wa barabara hiyo ambapo dola milioni
moja zitatolewa na serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwaajili ya kulipa
fidia kwa wananchi na zilizo bakia ni msada kutoka shirika la mafuta
ulimwenguni OPEQ.
Nae mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Bi. Mwanajuma Majidi Abdalla
amesema kumalizika kwa barabara hio nikiunganishi muhimu kati ya mkoa wa
kusini na kaskazini Pemba.
Ujenzi wa barabara hio ya Ole Kengeja ulianza 01.09.2014 hadi sasa
imefikia kilomter 11 tu kwakiwango cha kifusi inatarajia kutumia miezi
36 ya ujenzi wabarara hio tayari imekwisha tumia miezi 16 bado miezi 20
tu ambayo itajenga.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini