Mahakama
kuu ya Tanzania imetupilia mbali ombi la pingamizi la kuzuia kufanyika
kwa vikao vya mabaraza ya madiwani katika manispaa za Kinondoni na Ilala
jijini Dar es Salaam vitakavyotumika pia kuwachagua mameya katika
manispaa hizo.
Uamuzi huo wa mahakama kuu ya Tanzania umekuja kufuatia ombi la
mlalamikaji Bw Issay Charles diwani wa kata ya Vijibweni Temeke Dar es
Salaam ambaye aliiomba mahakama kusitisha vikao vya madiwani
vinavyotarajiwa kufanyika jan 09 katika manispaa za Ilala na Kinondoni
mpaka tafsiri sahihi ya kisheria itakapopatikana kuhusu uhalali za
wabunge wa Zanzibar kushiriki katika vikao vya madiwani vya Tanzania
bara, ambapo akisoma hukumu hiyo iliyochukua saa takribani nane kwa
niaba ya jopo la majaji watatu, jaji Lugano Mwandambo amesema hoja za
mlalamikaji hazina mashiko huku pia akimtaja mlalamikaji kuwa hana haki
ya kisheria kuingilia mambo ya manispaa hizo kwani hayamuhusu na kuagiza
vikao vya uchaguzi wa mameya katika manispaa hizo za Kinondoni la Ilala
zinapaswa kuendelea kama zilivyopangwa.
Awali wakili wa serikali Bw Gabriel Maratta aliithibitishia
mahakama uwepo wa wajumbe kutoka Zanzibar walioshiriki vikao vya
madiwani Dec 10 mwaka 2015 na kutoa ufafanuzi wa kina na wakisheria kwa
wajumbe hao kushiriki, na kuitaka mahakama kutupilia mbali ombi la
mlalamikaji kwani kushindwa kuapishwa kwa madiwani na uchaguzi wa mameya
umesababisha shughuli nyingi za serikali katika manispaa hizo kusimama
kwa kuwa hakuna baraza la madiwani ambalo hutumika kutoa maamuzi ya
utekelezaji wa masuala mbalimbali ya shughuli za serikali katika
manispaa hizo, huku shauri hilo likitarajiwa kutajwa tena mapema january
29 mwaka huu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini