Mashirika ya haki za binadamu yameripoti kuwa, machafuko hayo yaliyoanza
wiki kadhaa nyuma, yameshapelekea watu wasiopungua 140 kuuliwa na
vikosi vya serikali katika eneo la Oromia.
Shirika la Human Rights Watch lilitangaza jana (Ijumaa) kuwa, huo ni
mgogoro mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Ethiopia tangu ule wa
wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005.
Kwa mujibu wa shirika hilo, watu wengine wengi wamejeruhiwa kwenye machafuko hayo.
Human Rights Watch limeongeza kuwa, idadi ya wahanga wa machafuko hayo ni kubwa sana.
Hadi tunapokea habari hii, serikali ya Ethiopia ilikuwa imedai ni watu watano tu ndio waliouawa kwenye tukio hilo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini