
Akithibitisha kutokea kwa vifoo hivyo mganga mfawidhi wa hospitali
ya wilaya ya Manyoni Daktali Kitundu Jackson amekiri kupokea maiti hizo
ambazo zimeangukiwa na nyumba eneo la kitongoji cha kipondoda na
kuwataja walio kufa ni Amina Ashery miaka saba na Emily Ashery miaka
minne.
Akieleza huku akiwa na majonzi mama watoto hao wawili walio kufa
akiwa pamoja na watoto wengine watano walionusurika, amesema alikuwa
amelala yeye na familia yake na gafla alisikia kishindo na akafunikwa
na kifusi cha udongo ndipo alipoanza kuomba msaada, baada ya kutolewa
watoto wawili wakiwa katika hali mbaya na walipofika hospitali walikuwa
tayari wamesha fariki.
Kwa upande wake mkurugenzi wa mamlaka ya mji mdogo wilayani Manyoni
Bwana Yona Chalinze, amesema wao kama mamlaka walisha toa taarifa kwa
wenye viti wa mitaa kuwa watu wanao ishi mabondeni kuchuwa taadhari
kutokana na mvua kubwa zitakazo nyesha ,huku naye pia bi. Eliza mjengi
ambaye yeye alishuhudia alikuwa na haya yakusema.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini