
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha vipaumbele ambavyo vitatumika ili kuifanya elimu ya Tanzania kuwa bora na yenye manufaa kwa miaka ya mbeleni.
Alisema
kupitia kongamano hilo wamethibitisha ili kuwapo na elimu bora nchini
kunahitajika kuwa na walimu wenye sifa na ubora unaohitajika, mashuleni
kutumika vitabu vya ziada na kiada, kuimarisha huduma ya ukaguzi
mashuleni, watoto wote wenye umri wa kwenda shule wapelekwe shuleni na
kuwajengea uwezo wa stadi za kazi wahitimu ili hata wanapomaliza masomo
waweze kujiajiri.

“Tumethibitisha
yale maeneo muhimu ya sekta ya elimu ambayo tumegundua kwamba ili
tuweze kusonga mbele lazima tuimarishe ubora wa elimu yetu kama ni
walimu wasome vizuri wawe na ubora, tuwe na vitabu wanafunzi wapate
maarifa kutoka kwenye vitabu, kudhibiti ubora wa elimu na watoto waende
shule kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na elimu ya juu,”
alisema Tandari.
Aidha
Tandari alieleza kuwa awali walikuwa wakishindwa kuwa na mipango ya aina
hiyo kutokana na kutokuwepo kwa fedha lakini kwa sasa wataweza
kugharamia mpango huo wa elimu kutokana na serikali kuwa tayari
kusimamia mpango huo wa kuboresha elimu ya serikali.
Aliongeza
kuwa wao kama Wizara ya Elimu wanaamini kuwa mfumo wa elimu kwa sasa
utakwenda vizuri kutokana na kasi aliyonayo rais wa awamu ya tano, Dkt.
John Pombe Magufuli ambaye ameamua kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa
shule za msingi hadi sekondari na kutokana na kasi yake ya utendaji kazi
wanataraji utafanyika kama jinsi unavyopangwa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini