
Zaidi
ya wanafunzi 3000 wa shule za katoro na uhuru wanatumia matundu mawili
ya vyoo kutokana na vyoo vya awali kubomoka hivyo kusababisha usumbufu
mkubwa.
Akizungumza na ITV mwalimu mkuu wa shule ya msingi Katoro Paul Enos
amesema vyoo hivyo vimebomoka tangu mwaka jana hata hivyo uwingi wa
wanafunzi katika shule hizo zilizojirani unatokana na muitikio mkubwa wa
wanafunzi kuandikishwa hasa kufuatia ahadi ya rais wa jamuhuri ya
muungano wa Tanzania kuwa watoto wenye umri wa kwenda shule
kuandikishwa.
Katika kipindi cha mwaka wa masomo wa mwaka wa 2016, shule ya
msingi Katoro imeandikisha wanafunzi 497 na shule ya Uhuru imeandikisha
watoto 590 na bado wanapokea wanafunzi hadi marchi 31,ambapo mwaka jana
shule ya msingi Katoro iliandikisha wanafunzi 230 na Uhuru iliandikisha
wanafunzi 350 hivyo ongezeko ni kubwa kuliko mwaka jana.
Mpaka sasa halmashauri ya wilaya ya Geita imefikia asilimia tisini
ya uandikishwaji wanafunzi kwa shule za msingi ambapo, malengo ya
uandikishaji kwa mwaka huu ilikuwa ni wanafunzi 26154 lakini mpaka sasa
wameandikishwa 23731 na bado wanaendelea kuandikisha.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini