Wagonjwa 28 wa macho wafanyiwa upasuaji katika Hospitali ya rufaa JIJIN MWANZA. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Sunday, January 10, 2016

Wagonjwa 28 wa macho wafanyiwa upasuaji katika Hospitali ya rufaa JIJIN MWANZA.

Taasisi moja ya kidini mkoani Mwanza kwa kushirikiana na wafadhili kutoka nchini Kuwait, imetoa huduma ya bure ya upasuaji wa macho kwa wagonjwa 28 pamoja na kugawa miwani 258 kwa wananchi wenye matatizo ya macho waliofanyiwa uchunguzi katika kambi ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
Katibu wa taasisi hiyo ya chemchem Trust Fund Amir Said Amir amesema kuwa lengo la kutoa huduma hiyo bure ya miwani pamoja kuwafanyia upasuaji wagonjwa wenye matatizo ya ‘mtoto wa jicho’ ni kupunguza uoni hafifu katika jamii ya wakazi wa jiji la Mwanza.
 
Dk. Bahati Msaki ni mganga mfawidhi wa hospitali ya Sekou Toure, anatumia fursa ya kutembelewa na familia ya watu sita ya mfalme wa Kuwait Alswabah kueleza changamoto zinazoikabili idara ya macho ya hospitali hiyo, huku baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza nao wakieleza namna walivyonufaika na msaada huo.
 
Ujumbe huo wa familia ya kifalme, pia umezuru katika shule ya msingi maalumu ya Mitindo iliyopo wilayani Misungwi, ambayo ni kambi maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albino) na kutoa msaada wa vyakula kama vile mchele, mafuta na sukari pamoja na vifaa vya michezo na vya elimu ambapo mkuu wa wilaya hiyo Mwajuma Nyiruka amezitaja baadhi ya changamoto zinazokikabili.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin