Chadema yawataka Vijana wafanye KAZI na sio kuchangia MIGOGORO . . | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Sunday, January 10, 2016

Chadema yawataka Vijana wafanye KAZI na sio kuchangia MIGOGORO . .


Chadema yawataka vijana wafanye kazi na sio kuchangia Migogoro.
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Rukwa, kimewataka vijana wote ambao ni wanachama na washabiki wa chama hicho mkoani humo, watambue kuwa kipindi cha uchaguzi kimeshapita na wala sio wakati wa kutamani kufanya kampeni na maandamano,hali inayochangia kuwepo kwa migogoro ya mara kwa mara ndani ya chama, bali sasa waelekeze maisha yao katika kufanya kazi na uzalishaji.
Mwenyekiti wa chama cha chadema mkoani Rukwa Bw.Zeno Nkoswe, akiongea mjini Sumbawanga amesema wamebaini kuwa migogoro mingi na isiyoisha inayoendelea ndani ya chama hicho hivi sasa,ni vijana kutojitambua kuwa sasa kampeni zimeisha na uchaguzi umepita na kwamba kuna maisha baada ya uchaguzi,na wengi wanaojihusisha na migogoro hiyo ni wale walioshiriki kwenye kura za maoni,na pia ameeleza kuwa tofauti zao na makao makuu ya chama zilimalizwa na mratibu wa chama hicho kanda ya nyanda za juu Bw.Frank Mwaisumbe. 
 
Kwa upande wake katibu wa chadema wa wilaya ya Sumbawanga mjini Bw.Pius Nguvumali,amesema anashangazwa na kitendo cha waliokuwa wagombea ubunge katika majimbo ya kwela na nkasi kusini kupitia chama hicho, ambao sasa wamehamishia shughuli zao mjini hapa na kuchochea migogoro, wakati chama kikifanya tathmini ya ushiriki wao kwenye uchaguzi mkuu kujua walikosea wapi na kujipanga kwa upya.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin