Viongozi wa CCM wa Jumuiya za chama
hicho katika kata nane za jimbo la babati mjini mkoani Manyara
wameandamana kimyakimya na kujikusanya kwenye ofisi ya chama hicho
katika jimbo hilo wakishinikiza kulipwa deni la zaidi ya shilingi
milioni 18 la ruzuku ya posho za mabalozi na wenyeviti wa matawi
zilizotolewa na CCM makao makuu katika kipindi cha kampeni ya uchaguzi
mkuu kama malipo halali ya ruzuku ya posho za kukisaidia chama
hicho,huku wakitishia kukisaliti chama hicho endapo hawatalipwa.
Wakizungumza na ITV nje ya ofisi ya chama hicho baada ya kuwaita
mwenyekiti wa CCM wilaya na mjumbe wa halmashauri kuu-taifa na kuwabana
huku wakitaka majibu sahihi kati ya malipo ya awali ya shilingi milioni
48 yaliyotolewa na CCM makao makuu wamesema kabla ya uchaguzi mkuu
walisaini nusu ya malipo hayo ya shilingi milioni 30 lakini tangu
kumalizika kwa uchaguzi wamekuwa wakipigwa danadana na uongozi huo.
Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu Bw.Ali Khera Sumaye
alipotakiwa na wajumbe hao kutoa ufafanuzi ni lini watalipwa na CCM mara
kuwasili toka makao makuu ya CCM Dodoma alipokwenda kuupata ufafanuzi
amesema mpaka sasa mabalozi 300 hawajalipwa ruzuku ya posho zao ambazo
zimekwishalipwa na CCM makao makuu.
Hata hivyo mwenyekiti wa CCM wilaya ya Babati Bw.Ali Msuya
akizungumza baada ya katibu wake kuwepo safarini,amesema atafuatilia
mgogoro huo na kueleza kwamba hakushirikishwa na hafahamu kiasi gani
kilichotolewa na CCM makao makuu huku akidai kwamba chama kitawasiliana
na takukuru kuchunguza tuhuma hizo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini