Wafanyakazi wa kiwanda cha Play and Panel wamemuomba mkuu wa mkoa wa Tanga kuingilia kati mgogoro wa kimaslahi na mwekezaji wa kiwanda hicho. Wametoa malalamiko yao katika ziara ya mkuu wa mkoa ya kutembelea viwanda vilivyopo jijini Tanga. Ni mwendelezo wa ziraya ya mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwamtumu Mahiza ya kubainisha changamoto zinazowakabili wawekezaji na kuona namna ya kuzishughulikia. Katika kiwanda cha Play and Panel Mahiza anakutana na wafanyakazi wanaolalamikia kulipwa mshahara wa laki moja kwa mwezi, kiwango ambacho hata hivyo hazitoki kwa wakati. Akizungumzia malalamiko hayo Meneja usalishaji wa kiwanda hicho, Hamza Seleman anasema malalamiko hayo yanaweza kujibiwa na kiongozi wake wa juu ambaye yuko safarini. Hata hivyo mahiza ameagiza wafanyakazi hao kulipwa mishahara na stahiki zingine mara moja kwa kuwa wana haki kisheria. Migogoro ya kimaslahi ni moja kati ya changamoto zinazovikabili baadhi ya viwanda katika mkoa wa Tanga. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Friday, January 8, 2016

Wafanyakazi wa kiwanda cha Play and Panel wamemuomba mkuu wa mkoa wa Tanga kuingilia kati mgogoro wa kimaslahi na mwekezaji wa kiwanda hicho. Wametoa malalamiko yao katika ziara ya mkuu wa mkoa ya kutembelea viwanda vilivyopo jijini Tanga. Ni mwendelezo wa ziraya ya mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwamtumu Mahiza ya kubainisha changamoto zinazowakabili wawekezaji na kuona namna ya kuzishughulikia. Katika kiwanda cha Play and Panel Mahiza anakutana na wafanyakazi wanaolalamikia kulipwa mshahara wa laki moja kwa mwezi, kiwango ambacho hata hivyo hazitoki kwa wakati. Akizungumzia malalamiko hayo Meneja usalishaji wa kiwanda hicho, Hamza Seleman anasema malalamiko hayo yanaweza kujibiwa na kiongozi wake wa juu ambaye yuko safarini. Hata hivyo mahiza ameagiza wafanyakazi hao kulipwa mishahara na stahiki zingine mara moja kwa kuwa wana haki kisheria. Migogoro ya kimaslahi ni moja kati ya changamoto zinazovikabili baadhi ya viwanda katika mkoa wa Tanga.

            Wafanyakazi wa kiwanda cha Play and Panel wamemuomba mkuu wa mkoa wa Tanga kuingilia kati mgogoro wa kimaslahi na mwekezaji wa kiwanda hicho.
Wametoa malalamiko yao katika ziara ya mkuu wa mkoa ya kutembelea viwanda vilivyopo jijini Tanga.
 Ni mwendelezo wa ziraya ya mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwamtumu Mahiza ya kubainisha changamoto zinazowakabili wawekezaji na kuona namna ya kuzishughulikia.
          Katika kiwanda cha Play and Panel Mahiza anakutana na wafanyakazi wanaolalamikia kulipwa mshahara wa laki moja kwa mwezi, kiwango ambacho hata hivyo hazitoki kwa wakati.
           Akizungumzia malalamiko hayo Meneja usalishaji wa kiwanda hicho, Hamza Seleman anasema malalamiko hayo yanaweza kujibiwa na kiongozi wake wa juu ambaye yuko safarini.
Hata hivyo mahiza ameagiza wafanyakazi hao kulipwa mishahara na stahiki zingine mara moja kwa kuwa wana haki kisheria.
Migogoro ya kimaslahi ni moja kati ya changamoto zinazovikabili baadhi ya viwanda katika mkoa wa Tanga.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin