Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limewataka madereva
wa mabasi ya abiria yanayokwenda mikoa inayopakana na nchi zenye
machafuko kuhakikisha kuwa wanabeba abiria na mizigo ambayo ni salama,
kutokana na ongezeko la uingizwaji wa silaha na wahamiaji haramu
wanaotumia usafiri huo.
Inaelezwa kuwa silaha nyingi zimekuwa zikitoka mikoa iliyopakana na nchi kama Burundi, Congo DR na Kenya, ambayo ina mahusiano hasimu na kundi la kigaidi la Al Shabaab la nchini Somalia.
Kamanda Simon Sirro kwa mara ya kwanza tangu kushika wadhifa wa kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, amekutana na madereva wa mabasi hayo Jijini Dar es Salaam, ambapo alianza kwa kuwataka madereva kuhakikishia usalama wao, abiria na mizigo inayosafirishwa.
Amewataka kutoa taarifa kwa jeshi hilo haraka iwapo watamtilia shaka abiria ama mzigo wowote ili kupunguza usafirishaji wa silaha.
Kuhusiana na dawa za kulevya, Kamanda Sirro amesema, japo inaelezwa kuwa dawa nyingi zinapitia kwenye maji, lakini bado madereva nao wana nafasi muhimu katika kuhakikisha biashara hiyo haramu inadhibitiwa, kwa kutoa taarifa mapema.
Kumekuwepo na ongezeko la matukio ya uhalifu kwenye maeneo mbalimbali nchini, hususan kwenye majiji makubwa, kutokana na ongezeko la silaha zinazotoka kwenye nchi hizo za jiran.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini