Halmashauri ya Wilaya Hai yapiga marufuku kuwaajiri walimu. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Friday, January 8, 2016

Halmashauri ya Wilaya Hai yapiga marufuku kuwaajiri walimu.

Halmashauri ya wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro imepiga marufuku taasisi binafsi za elimu wilayani humo kuajiri walimu ambao hawana taaluma ya ualimu na kuwataka walimu hao kujiendeleza mara moja kitaaluma.
Hatua hiyo inalenga kudhibiti ongezeko la walimu wasio na sifa ya ualimu sababu hiyo ikitajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi wengi kutokuwa na nidhamu na maadili mema.
Kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Hai Bwana Said Mderu wakati akizungumza  na wamiliki wa shule binafsi na  na vyuo  wilayani humo ,katika kikao elekezi kilicholenga kutoa taswira halisi ya mwaka mpya wa masomo 2016.
Pamoja na hatua hiyo ,Mderu pia ameonya  kuajiri watumishi kutoka nje ya nchi ambao hawana kibari cha kufanya kazi nchini Tanzania.
Kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu  wametumia fursa hio kuzitaka taasisi za elimu wilayani humo  kutoa elimu bora itakayowawezesha  wanafunzi kujitegemea katika maisha yao ya baadae.
Katika kikao hicho imebainika kuwa kati ya shule 16 za wamiliki binafsi, ni shule mbili pekee ndiyo zinatajwa kuwa na walimu wenye taaluma kamili.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin