Mwanasiasa
mkongwe nchini, Kingunge Ngombare Mwiru, amesema atampima na
kuzungumzia utendaji wa Rais wa tano, John Magufuli atakapotimiza siku
100 Ikulu.
Dk.
Magufuli leo ametimiza siku 59 tangu kuapishwa kushika madaraka hayo
Novemba 5, mwaka jana na ameshafanya mambo makubwa yaliyompa sifa kem
kem kitaifa na kimataifa.
Kingunge
ambaye mwishoni mwa mwaka jana alikihama chama alichokiasisi cha CCM na
kukitumikia kwa zaidi ya miaka 60, jana alisema kwa kawaida watu
hupimwa utendaji wao wa kazi zinapofika siku 100.
Kingunge
ambaye alikuwa na kadi namba 8 CCM kabla ya kujiunga na Umoja wa Katiba
ya Wananchi kumpigia kampeni aliyekuwa mgombea wa Chadema kwenye
Uchaguzi Mkuu, Edward Lowassa, alisema ni mapema mno kujadili utendaji
wa serikali ya Magufuli.
“Jamani
nadhani ni mapema mno, msiwe na haraka nitatoa maoni yangu kuhusu
utendaji wake muda huo utakapofika. Kwa sasa mwacheni afanye kazi zake
msimwingie ingilie," alisema Kingune ambaye amewahi kushika nyadhifa nzito nzito serikalini.
"Kwani nyinyi mna haraka gani mpaka mnataka nitoe maoni yangu leo?" Aliuliza. "Bado ni mapema sana kumpima.”
Kingunge alisisitiza kuwa ni vyema Magufuli akaachwa afanye kazi zake kwa sasa.
Oktoba
4, mwaka jana, Kingunge alitangaza rasmi kujiengua ndani ya chama
hicho, akisema alifanya hivyo kutokana na kile alichoamini kuwa CCM
haifanyi yale yaliyoasisiwa na kujengewa misingi bora na waasisi wake.
Wakati
akitangaza uamuzi huo, Kingunge alisema hakusudii kujiunga na chama
chochote cha siasa nchini bali atakuwa mtanzania huru, lakini muda si
mrefu akaungana na Ukawa kumnadi Lowassa.
Mwanasiasa
huyo ambaye sehemu kubwa ya maisha yake alikuwa CCM, alisema wananchi
wanataka mabadiliko na wasipoyaona ndani ya chama hicho watayatafuta nje
ya chama, ikiwa ni nukuu ya nasaha maarufu ya Baba wa Taifa, hayati
Julius Nyerere aliyowahi kuitoa enzi za uhai wake.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini