Baadhi
ya wakuu wa vituo vya afya na zahanati katika Manispaa ya Bukoba,
wamegoma kupokea misaada kwa ajili ya wajawazito uliotolewa na Mbunge wa
Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare kwa madai ya kupewa maelekezo
na Serikali.
Mbunge
huyo mwishoni mwa wiki alikuwa akisambaza vifaa tiba katika vituo vya
afya na zahanati, lakini wasimamizi walikataa kuvipokea, huku wengine
wakikimbia wakidai walipewa maelekezo na viongozi wao kutovipokea.
Katika
hali ya kushangaza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Richard
Mihayo ambaye alikuwa katika msafara wa mbunge huyo alitoweka ghafla
baada ya kufika Kituo cha Afya cha Zamzam, huku Kaimu mganga, Samwel
Chaba akigoma kupokea vifaa hivyo.
Baada
ya mkurugenzi kutoweka, mbunge huyo alilazimika kutelekeza vifaa hivyo
kituoni hapo na kwenda Zahanati ya Kashai ambako Kaimu Msimamizi wa
zahanati hiyo, Emmanel Luviga alikubali kuvipokea.
Katika Kituo cha Afya Rwamishenye vifaa hivyo vilipokewa na wauguzi waliogoma kuzungumza suala lolote.
Baada
ya kufika Zahanati ya Kagemu, Msimamizi wake Glory Sailo aligoma
kupokea vifaa kwa ajili ya mama wajawazito kwa madai ni maelekezo ya
viongozi.
Hatua
ya viongozi kuweka vikwazo kwenye upokeaji wa vifaa hivyo vyenye
thamani ya zaidi ya Sh3 milioni ililalamikiwa na Lwakatare aliyedai
aliandika barua manispaa na kutoa nakala hadi ngazi ya mkoa, lakini
Mganga Mkuu wa manispaa hiyo, Dk Hamza Mgula alisema hajui lolote kuhusu
suala hilo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini