Rais Magufuli Amtembelea Na Kumfariji Mama Maria Nyerere Kufuatia Kufiwa na Mkwewe Bi Leticia Nyerere . | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Monday, January 11, 2016

Rais Magufuli Amtembelea Na Kumfariji Mama Maria Nyerere Kufuatia Kufiwa na Mkwewe Bi Leticia Nyerere .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Januari, 2016 amemtembelea na kumpa pole mke wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere kufuatia kifo cha Mkwewe Leticia Nyerere kilichotokea jana huko Maryland Marekani alikopelekwa kwa ajili ya kupata matibabu mapema mwezi huu.


Pamoja na kutoa mkono wa pole kwa Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani Jijini      Dar es Salaam, Rais Magufuli pia amewapa pole wanafamilia wote na amewaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na ndugu yao.

Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere Bwana Joseph Butiku amemueleza Rais Magufuli kuwa familia inaendelea na taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Marekani na itatoa taarifa baadaye.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
11 Januari, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mama Maria Nyerere kufatia kufiwa na Mkwe wake Bi Leticia Nyerere aliyefariki huko nchini Marekani. Rais alikwenda nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani Dar es salaam kumpa pole Mama nyerere Januari 11,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapa pole wanafamilia alipofika nyumbani kwa Baba wa Taifa Msasani Dar es salaam kumpa pole Mama nyerere Januari 11,2016
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo juu ya uataratibu wa msiba kutoka kwa mwanafamilia Joseph Butiku
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wanafamilia
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Mama Maria Nyerere, Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, na wanafamilia alipokwenda nyumbani kwake Msasani kumfariji kufuatia kifo cha Mkwe wake Marehemu Leticia Nyerere huko Maryland, Marekani.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin