Hatua hiyo inakuja ikiwa tayari zaidi ya watu 12,000 wameripotiwa kuugua ugonjwa wa kipindupindu na wengine kufariki dunia chanzo kikitajwa kuwa ni ulaji wa chakula kisicho salama.
Meneja Mawasiliano na uhusiano wa Umma- TFDA Gaudensia Simwanza amesema kasi ya ongezeko la magonjwa yatokana na sumu kwenye chakula ni kubwa hivyo zoezi hilo litaenda sambamba na kuwachulia hatua wale wote watakaobanika kuuza chakula kisichochunguzwa na Mamlaka hiyo.
Amesema kuna sababu nyingi zinazopelekea mtumiaji wa chakula kisicho salama kupata madhara ikiwa pamoja na kula chakula chenye sumu kuvu,takataka katika chakula na uchafuzi wa vimelea vya maradhi katika chakula na hapa anaeleza mkakati wa kubaliana na athari hizo.
Aidha amesema uhitaji wa TFDA kuzuia chakula chenye madhara kufika kwa mlango ni changomoto inayokabili inayosababishwa na mifumo ya kukosekana takwimu sahihi za watu waliyoathirika kutoka na ulaji wa chakula.
Hadi sasa tayari TFDA imekwisha anza kukusanya takwimu za kisayansi ili kubaini madhara yanayosababishwa na chakula, mpango unaofanyika katika mikoa saba na kubaini watu 7 349 walipatwa na magonjwa ya kuharisha ,homa ya matumbo, kuhara damu, minyoo, amiba, kipindipindu, sumu katika chakula na Brusela yote magonjwa yote yalisabishwa na ulaji wa chakula.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini