Iman potofu kikwazo Cha matibabu Kwa Watoto walemavu. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Monday, January 11, 2016

Iman potofu kikwazo Cha matibabu Kwa Watoto walemavu.


Uelewa mdogo kwa jamii na imani potofu juu ya maradhi ya mguu rungu wanayopata watoto wanapozaliwa ni miongoni mwa sababu zinazochangia idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa nchini kupata ulemavu.
Maatizo hayo ambayo kwa kiasi kikubwa matibabu yake huchukuwa muda mrefu, huwa na kikwazo zaidi pale mzazi anapochelewa kumfikisha hospitali mtoto wake aliyezaliwa na maradhi hayo.
Ukubwa watatizo hilo hapa nchini limeipelekea Jumuya ya  Zanzibar out reach Programe ZOP kwa kushirikiana na kitengo cha  mifupa na viungo katika hospitali kuu ya mnazi mmoja visiwani hapa kuendesha mafunzo  kwa madaktari  ili kupata wataalamu wengi zaidi watakaowasaidia wanajamii wanaopata matatizo hayo.
Akizungumza  na wanahabari  mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo mtaalamu wa matibabu ya watoto wenye mguu rungu hospitali ya mnazi mmoja Salim Seif Ali anasema ni vyema jamii ikaelewa matatizo hayo yanatibika  na wajenge utamaduni wa kuwahisha hospitalini.
Daktari bingwa wa mifupa na viungo bandia ambae ndie mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka hospitali ya Bugando JIJINI mwanza DR ISDOR  NGAYOMELA  anasema  uchumi mdogo kwa baadhi ya jamii za kuweza kufuatilia matibabu sambamba na uelewa mdogo huchangia matatizo hayo ila kupitia mafunzo hayo itasaidia kuwasambaza wataalamu watakaosaidia kupunguza tatizo hilo.
Mafunzo hayo ya siku mbili yatasaidia sana kupunguza ukubwa wa tatizo visiwani na hata maeneo mengine Tanzania.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin