Mkuu wa wilaya ya Kiondoni Paul Makonda amewataka wakazi wa eneo
lake kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi wa shule za sekondari ili ziweze
kukidhi mahitaji ya wilaya hiyo, huku akisisitiza juhudi zaidi ili
ifikapo mwezi March mwaka huu, shule hizo ziwe zimekamilika.
Wilaya ya Kinondoni kama ilivyo kwa wilaya nyingine, inakabiliwa na upungufu wa shule, hatua inayosababisha wanafunzi wengine kusoma mbali na maeneo wanayoishi na kuwasababishia usumbufu mkubwa.
Wilaya ya Kinondoni imeanza utekelezaji wa ujenzi wa shule zinazotarajia kuziba pengo lililopo la upungufu wa shule, na kusababisha adha kubwa kwa wanafunzi, hususani ya kusoma mbali na makazi yao, na wengine kukosa fursa ya elimu.
Mkuu wa wilaya hiyo Paul Makonda, alizindua rasmi ujenzi wa majengo ya shule hizo, ambazo tayari zimekwishaanza kujengwa, pamoja na mambo mengine aliwataka wananchi kuongeza ushirikiano, kwa kuwa tayari serikali imebeba jukumu la kusomesha bure watoto wao.
Pamoja hayo mkurugenzi wa Manispaa hiyo, ambaye yeye akawataka wakazi wa Kinondoni kujenga majengo hayo kwa kuweka nia ya kuwawezesha watoto waliokosa shule, kuanza masomo ifikapo mwezi wa tatu.
Ukosefu wa shule hizo umesababisha wanafunzi wengi kukosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza, na maeneo yenye uhaba ni katika kata za Mzimuni, Ubungo, Kimara, Kinondoni, Magomeni na Mbezi juu.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini