Waziri
wa afya, wazee, jinsia na watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu amezindua
mpango wa huduma za madaktari bingwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa
wa Ruvuma unaoratibiwa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) ambao
watatoa huduma za magonjwa mbalimbali kwa siku saba huku akisema serikali inajipanga kuhakikisha matibabu kwa bima ya afya yanakuwa ya lazima.
Waziri wa afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu amezindua mpango huo mkoani
Ruvuma ulioendana mfuko wa taifa wa bima ya afya kutoa vifaa tiba kwa
hospitali hiyo pamoja na mashuka 360 wakati ambao taifa linakabiliwa na
upungufu mkubwa wa madaktari bingwa ambapo daktari mmoja anahudumia
wagonjwa thelasini elfu wakati inatakiwa daktari bingwa mmoja awahudumie
wagonjwa elfu moja.
Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa taifa
wa bima ya afya (NHIF) Bw. Michael Mhando anasema lengo la mpango huo
ni kufikisha huduma za matibabu kwa mikoa ya pembezoni badala ya kutumia
gharama kubwa kufuata huduma za madaktari bingwa mbali na mikoa yao.
Zaidi kuhusiana na madaktari hao
watano bingwa wa magonjwa mbalimba ambao watatoa huduma kwa siku saba
mkoani Ruvuma mkurugenzi wa mfuko wa afya ya jamii(CHF) Bw.Ugin
Mikongoti ana haya ya kusema.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini