NAIBU Aibua madudu Kiwanda cha Nondo Mwanza. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Monday, January 11, 2016

NAIBU Aibua madudu Kiwanda cha Nondo Mwanza.


Serikali imeonya kukifunga kiwanda cha uzalishaji wa nondo cha Nyakato Steel jijini Mwanza ndani ya muda wa wiki mbili kuanzia leo endapo uongozi wa kiwanda hicho utashindwa kuzoa na kuvirundika sehemu sahii vyuma vilivyozagaa ovyo katika eneo la kiwanda hicho.
Naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais mazingira na muungano Mh Luhaga Mpina ametoa onyo hilo mapema jana alipotembelea kiwanda hicho ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Mwanza.
 Ziara ya kukagua na kujiridhisha juu ya zoezi la usafi wa mazingira linavyo tekelezwa jijini Mwanza inamfikisha Naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira na muungano katika kiwanda cha kuzalisha nondo cha Nyakato.
Shehena  ya vyuma ambavyo ni malighafi ya uzalishaji wa bidhaa hizo ni yenye kutia shaka afya za wakazi wanao zunguka eneo la kiwanda hicho.
Kutokana na kile kinacho elezwa kuwa ni maji yanayobeba kemikali pindi vyuma hivyo vinaponyeshewa mvua na kutiririshi maji  katika makazi na vyanzo vya maji vinavyo zunguka eneo hilo.
 Ni agizo lililoenda sambamba na mwito kwa balaza la mazingira la taifa Nemc kanda ya Mwanza kufanya uchunguzi dhidi ya athari za moshi mzito unaodaiwa kuzalishwa na kiwanda hicho nyakati za usiku.
 Pamoja na mambo mengine ziara ya naibu waziri Mpina inalenga kutazama uzingatiwaji wa sheria na kanuni za uhifadhi wa mazingira viwandani pamoja na kuhamasisha upandaji miti katika halimashauri mbalimbali ili kufikia lengo la kila halmashauri kupanda miti milioni 1.5.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin