Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi-OSHA, itafanya msako
nchini kote na kuwafikisha mahakamani wamiliki wa taasisi za umma na
binafsi watakaobainika kuwa hawajakamilisha usajili katika chombo hicho.
Mkurugenzi wa OSHA, Dokta Akwilina Kayumba, amesema msako huo
utafanyika baada ya kumalizika kwa muda wa siku 14 zilizotolewa na
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira,Vijana na
Walemavu, Jenista Mhagama la kumtaka kila mmiliki kuwa na kibali cha
OSHA.Dakta Akwilina Kayumba, Mtendaji Mkuu wa OSHA ameelezea namna chombo hicho kitakavyoanza kutekeleza matakwa ya kifungu cha 16(1) cha sheria ya usalama na afya mahala pa kazi ya mwaka 2003
Amesema sheria ya OSHA inamtaka kila mwajiri kuhakikisha anasajiliwa na chombo hicho kabla ya kuanza uzalishaji, hivyo amewataka wahakikishe wote wanatekeleza matakwa ya sheria hiyo kabla ya msako huo kuanza.
Takwimu zilizotolewa na OSHA, tangu kutolewa agizo hilo hadi sasa idadi ya usajili sehemu ya kazi imeongezeka kwa zaidi ya mara mbili, wakati usajili kabla ya agizo la waziri ilikuwa ni taasisi 60 kwa wiki, lakini baada ya agizo kila wiki makampuni 150 yanasajiliwa na sheria hiyo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini