Idara ya Uhamiaji Yawakamata12 mbaroni mkoan Shinyanga Raia wa BURUNDI. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Friday, January 8, 2016

Idara ya Uhamiaji Yawakamata12 mbaroni mkoan Shinyanga Raia wa BURUNDI.


wahamiaj


       Idara ya Uhamiaji mkoani Shinyanga imewakamata vijana 12 ambao ni wahamiaji haramu kutoka nchini Burundi wakijihusisha na shughuli za ubebaji wa abiria kwa kutumia Baiskeli na Pikipiki wilayani Kahama.
      Wimbi la wahamiaji haramu nchini linazidi kushika kasi katika wilaya ya Kahama ambapo ajira za wazawa za usafirishaji maarufu kama bodaboda zinadaiwa kuporwa na wahamiaji hao ambao wanadaiwa pia kujihusisha na vitendo vya uhalifu.
      Baiskeli na Pikipiki ndio usafiri unaotegemewa wilayani Kahama ,kutokana na kukosekana kwa usafiri wa ndani wa mabasi maarufa kama daladala ,wakazi kulazimika kutumia Baiskeli na Pikipiki
Baadhi ya wahamiaji haramu utumia nafasi hiyo kupenye na kufanya shuhguli hizo  ili kujimilikisha uzawa usio rasmi, Idara ya uhamiaji  mkoani Shinyanga imewanasa wahamiaji haramu  wilayani Kahama.
Baadhi ya wahamiaji hao wamekiri kuingia Nchini kinyemela na kufanya shughuli za mbalimbali kwa  kivuli cha wazawa.
    Wilaya ya Kahama imekuwa na mwingiliano mkubwa wa watu kutoka Nchini jirani kufuati   kushamili kwa shughuli za kiuchumi katika ukanda wa Africa mashariki.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin