Watuhumiwa katika kesi hiyo ni alieyekuwa mwenyekiti wa Halmashauri Paulo Magazi,Zuberi Ndokezi,Juma Itengesha,Edward Kalikali wengine Bahati Shitagata ,Yared Nyanda na Clistina Ntelya katibu wa mikutano Msaidizi.
Kesi hiyo imefunguliwa na taasisi ya kuzuia Rushwa ambapo madiwani hao wanadaiwa kila mmoja kujipatia shilingi laki 160.000 za kikao
Mahongo ambae kwa sasa mkurugenzi wa Manspaa ya Morogoro alitinga Mahakamani kutoa ushaidi juu ya mashitaka ya madiwani wakati wa kipindi cha ukurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Kahama.
Katika ushaidi wake alisema anaimani kwamba mtuhumiwa wa kwanza ambaye alikuwa mwenyekiti wa Halmashauri bw Paul Magazi 13,9,2009 aliongoza kikao cha baraza la madiwani huku yeye akiwa katibu wa kikao
Hata hivyo ubishani mkubwa wa mawakili wa upande wa mashitaka na utetezi ulikuwa pale kwenye malipo ambapo magazi sahihi yake ilionekana kwenye hati ya malipo
Wakati katika daftari la mauzulio jina lake alikuwepo sanjali na watuhumiwa wengine majina hayakuwepo kwenye daftari lakini kwenye hati ya malipo sahihi zao zilikuwepo kesi hiyo itatajwa feb 6 na watuhumiwa wako nje kwa dhamana.
Wakati huo huo wafanya biashara 2 wakazi wa Kahama wamefikishwa Mahakamani kwa makosa ya kugushi nyaraka za mgodi wa Acacia na kuiba saluji yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 320
Watuhumiwa hao ni Hafidh Luhaga na Noa Charles Ambao wanadaiwa kumuibia mlalamikaji bw Ahamed Gulamrasuly mkazi wa Kahama kesi hiyo iliyotajwa tarehe January 20 mwaka huu mkoan hapo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini