Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP Simoni Haule
amesema ajali hiyo ambayo imehusisha basi la Mohamed Trans lenye usajili
wa namba T.858 AWY Scania iliyokuwa ikitokea Mwanza na kuelekea jijini
Dar-es-Salaam, baada ya kugonga kingo ya daraja katika mlima Sekenke
wilayani Iramba.
Katika hatua nyingi kamanda Haule amesema chanzo cha ajali hiyo ni
hitilafu ya usukani wa basi hilo na hivyo kupelekea dereva wa basi hilo
Bwana Jovin kushindwa kulimudu na kugonga kingo za barabara na
kusababisha kifoo na majeruhi.
Kamanda Haule amewataka madereva na wamiliki wa mabasi kuwa makini
kuhakikisha mabasi yao wana yafanyia matengenezo mara kwa mara ili kuepusha ajali wakiwa safalini.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini