Askofu wa kanisa la Anglikana dayosisi ya Victoria Nyanza afukuzwa kazi kwa ubadhirifu wa fedha. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Sunday, January 10, 2016

Askofu wa kanisa la Anglikana dayosisi ya Victoria Nyanza afukuzwa kazi kwa ubadhirifu wa fedha.

Zaidi ya wachungaji hamsini wa kanisa la Anglikana Tanzania dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN) wametangaza kumfukuza kazi ya uaskofu, askofu Bonifasi Kwangu wa dayosisi hiyo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha pamoja na mali za kanisa hilo.
Tamko hilo la wachungaji 53 wa dayosisi hiyo limesomwa mbele ya waumini wa kanisa kuu la mtakatifu Nicholas wakati wa ibada ya jumapili na mchungaji Andrew Kashilimu, ambaye pia ni mwenyekiti wa nyumba ya wahudumu.
 
Kufukuzwa kazi ya uaskofu kwa askofu Bonifasi Kwangu aliyehudumu katika dayosisi hiyo ya Victoria Nyanza (DVN) kwa miaka minane, kuanzia mwaka 2008 hadi kufikia leo, kunafanya jumla ya maaskofu waliowahi kufukuzwa na kanisa hilo kufikia wawili, akiwemo mtangulizi wake marehemu John Changaye ambaye alifukuzwa uaskofu mwaka 2007 kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha na mali za kanisa hilo.
 
Askofu Bonifasi Kwangu amevuliwa wadhifa huo akiwa nchini Marekani ambako amekaa kwa zaidi ya mwezi mmoja.
 
Kanisa la Anglikana Tanzania dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN) lina jumla ya wachungaji sitini na zaidi ya waumini laki sita katika makanisa yake.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin