WIZARA
ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema operesheni kwa lengo la kuwachukulia
hatua raia wa nje wanaofanya kazi nchini bila kufuata sheria za nchi, ni
endelevu na itagusa maeneo yote ikiwemo wafanyakazi wa majumbani.
Msemaji
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga, jana alisema hawakukurupuka
kuendesha operesheni hiyo, bali hakuna mgeni anayeruhusiwa kufanya kazi
nchini bila vibali.
Tamko
hilo la kusisitiza limekuja huku takwimu zikionesha kwamba, hadi
mwishoni mwa wiki, watu 79 walishakamatwa na Idara ya Uhamiaji kwa kosa
la kuishi nchini bila vibali na kufanya kazi wasizo na taaluma nazo.
“Lengo
la Wizara ni kuhakikisha operesheni hii inaenda kwa kasi na kwa
ufanisi, tutagusa maeneo yote, iwe viwandani, mashambani na hata
majumbani lazima lengo letu litimie,” alisema Nantanga.
Alisisitiza, “Nawatahadharisha
wale wote wanaodai kuwa tumekurupuka, watambue kuwa hakuna mgeni yeyote
anayeruhusiwa kufanya kazi nchini kinyume cha Sheria, hivyo wale wote
wanaoendelea kuwaajiri wageni wa aina hiyo wamevunja Sheria.”
Alisema
Serikali inafanya kazi kuhakikisha nchi inakuwa salama na watu wote
wanafuata Sheria. Alisema kuendelea kuwepo kwa raia wa kigeni wanaofanya
kazi bila vibali ni kuvunja Sheria.
Aliwataka
raia wa kigeni wanaotambua kuwa wanafanyakazi kinyume cha sheria,
ikiwemo kutokuwa na vibali, kujisalimisha wenyewe ofisi za Uhamiaji
kabla ya kufikiwa na operesheni hiyo.
Aidha
aliwataka waajiri wote kuhakikisha raia wote wa kigeni waliowaajiri
wanafanya kazi kihalali. Alisisitiza, endapo kuna raia wa kigeni asiye
na kibali au yuko kinyume cha Sheria, asalimishwe Uhamiaji mara moja
kabla sheria haijachukua mkondo wake, au kuwasili sha taarifa zake.
Alitoa
mwito kwa wananchi wenye taarifa za kuwepo kwa raia wa kigeni,
wanaoishi au kufanyakazi kinyume cha sheria, kuziwasilisha wizarani
ziweze kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.
“Natoa
onyo, watu wasije wakajificha na kudhani kuwa wako salama kwa sababu
operesheni hii ni endelevu, popote walipo tutawafikia,” alisema.
Hadi
mwishoni mwa wiki watu 79 walishakamatwa na Idara ya Uhamiaji kwa kosa
la kuishi nchini bila vibali na kufanya kazi wasizo na taaluma nazo.
Kwa mujibu wa Naibu Kamishna wa Uhamiaji Dar es Salaam, John Msumule, watuhumiwa hao wanatoka katika nchi 15.
Nchi
hizo na idadi ya waliokamatwa kwenye mabano ni Nigeria (4), China (20),
Ethiopia (23), Korea (9), Jamhuri ya Kidemokrasia ya CongoDRC (6),
Somalia (3),Uganda (2), Madagascar (5), Burundi (2), Ivory Coast (1),
Lebanon (1), India (1), Zimbabwe (1) na Ghana (1).
Hivi
karibuni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni
alipofanya ziara Makao Makuu Idara ya Uhamiaji, aliagiza ichunguze
kampuni zote nchini zinazotoa ajira kwa wageni wakati ajira hizo
wangeweza kupewa Watanzania wenye sifa.
Masauni
aliwaambia watendaji wakuu wa idara hiyo kwamba lazima kuwe na mfumo
thabiti wa kudhibiti tatizo hilo kwa ajili ya manufaa ya nchi nzima.
Aliagiza
idara hiyo kuimarisha ulinzi na ukaguzi wa mipaka nchini, kurahisisha
mapambano dhidi ya wageni wanaoingia nchini kiholela.
Hata
hivyo, alitaka idara hiyo kushughulikia haraka tatizo la vibali vya
ukazi, kwa kile alichosema imebainika kuwepo wakazi wengi wa kigeni
nchini waishio na kufanya kazi nchini kinyume na sheria za nchi
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini