KATIBU
Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, leo
anatarajia kufichua siri ya mazungumzo ya kusaka suluhu, baada ya
matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kufutwa mwaka jana.
Maalim
Seif, anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari leo saa tano asubuhi kueleza hatima
ya mazungumzo ya kisiasa ya kutafuta mwafaka Zanzibar
“Maalim Seif kesho (leo), atazungumza na wahariri na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa mazungumzo ya maridhiano Zanzibar,” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana.
Seif
anachukua uamuzi huo wakati hali ya kisiasa visiwani humo ikizidi kuwa
ngumu kwa pande zote, licha ya Rais Dk. John Magufuli kuahidi kuupatia
ufumbuzi mgogoro huo.
Maalim
Seif anajitokeza leo, wakati wiki iliyopita Rais Magufuli alikutana
na viongozi wastaafu, ambao kwa pamoja walizungumza mambo mazito ya
kitaifa pamoja na kutakiana heri ya mwaka mpya.
Wiki
iliyopita Rais Dk. Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Rais
mstaafu, Benjamin Mkapa ambaye alimhakikishia kumpa ushirikiano
atakapohitajika kufanya hivyo.
Katika
kumhakikishia kuwa yuko tayari kufanyakazi atakayomtuma, taarifa za
ndani zinaeleza kuwa moja ya jambo kubwa ambalo Mkapa anaweza
kulisimamia ni suala la kusaka suluhu ya Zanzibar.
Akizungumza
baada ya mazungumzo hayo, Mkapa alisema lengo la mkutano huo ni
kumpongeza Rais Dk. Magufuli kwa dhamana aliyopewa na Watanzania na
kumtakia heri ya mwaka mpya.
Mkapa
alimhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati
wowote na kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo.
Licha
ya Mkapa, Rais Magufuli pia alikutana na Rais mstaafu wa awamu ya nne,
Jakaya Kikwete, ambaye alikabidhi baadhi ya nyaraka kwa Rais Magufuli.
Kikwete
alikabidhiwa nyaraka hizo zinazohusiana na mgogoro huo na aliyekuwa
mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif
Sharif Hamad, Novemba 4, mwaka jana.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini