Ujenzi wa eneo la shuguli za uuma waaza bonde la Msimbazi. | nyula blog

Habari Kila Pande

Breaking News
Loading...

Monday, January 11, 2016

Ujenzi wa eneo la shuguli za uuma waaza bonde la Msimbazi.

Serikali imeanza kutekeleza Mradi wa Ujenzi wa eneo la shughuli za umma kwa kuondoa vifusi kwenye bonde la mto Msimbazi eneo la Mkwajuni hadi Jangwani jijini Dar Es Salaam.
Utekelezaji huo umelenga kuendeleza maeneo ya mabondeni kwa kutekeleza miradi ya umma yenye kukidhi eneo la mabondeni badala ya kuruhusu makazi ya watu ambayo yameonekana kuwa hatarishi zaidi.
Mradi huo umefatia siku chache baada ya serikali kusitisha shughuli ya bomoabomoa kwenye maeneo mbalimbali isipokuwa katika eneo la Bonde la Mto Msimbazi ambalo hata hivyo bomoabomoa itaendelea kwa utaratibu ambao hautaleta madhara kwa wananchi.
Katika ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba anabainisha kuwa mradi huo ni kwa maslai ya wananchi wote na kwamba lengo la serikali ni kuokoa maisha ya wananchi wake kwa kuwaondoa sehemu hatarishi.
Licha ya utekelezwaji wa mradi huo kwenye eneo hilo kuanza lakini bado wakazi wa eneo hilo wanaendelea kuishi.
Hata hivyo Waziri Makamba anawatoa hofu wananchi hao kwamba lengo la serikali si kuumiza wananchi wake na kuamua kuziagiza serikali za mtaa kuhakiki wakazi hao kwajili ya kupatiwa haki zao stahiki kwa mujibu wa sheria.
Tangu kuanza kwa shughuli hiyo Mapema Desemba 17 Mwaka jana, hadi sasa tayari nyumba 774 zimebomolewa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin