Waziri huyo wa mambo ya ndani ametoa agizo hilo mara baada ya
kutembelea makao makuu ya ofisi za zima moto jijini Dar es Salaam na
kuwasisitiza viongozi wote wa kikosi cha zima moto nchini kuhakikisha
wanaboresha huduma zao ili ziendane na kasi ya mababiliko ambayo
serikali ya awamu ya tano inakwenda nayo licha ya kikosi hicho
kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa vitendea kazi ambapo
waziri Kitwanga amekiri kufahamu changamoto hizo.
Kwa upande wake kamishina jenerali wa kikosi cha jeshi la zima moto
nchini Bwana Pius Nyambacha mbali na kukiri kikosi chake kukabiliwa na
changamoto ya vitendea kazi nahasa wakati huu wa mabadiliko ya ujenzi wa
nyumba za maghorofa kupata shida kuzima moto wakati wa majanga ya moto
hivyo ameiyomba serikali kutenga fedha za kutosha katika bajeti hususani
manunuzi ya vifaa vya kuzimia moto.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini