Baraza
la Mitihani la Tanzania limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali
wakiomba ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya
kijamii kuwa limebadilisha Viwango vya Ufaulu (Grade Ranges).
Baraza
la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watahiniwa na umma kwa
ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kupotosha umma na
kuleta taharuki.
Hivyo,
Baraza linaomba umma kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa Baraza halijafanya
mabadiliko yoyote kuhusu Viwango vya Ufaulu vinavyotumika sasa.
Imetolewa na,
AFISA HABARI NA UHUSIANO
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini