Chama cha kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi Tanzania (URA) kimetumia zaidi ya shilingi bilioni themanini kukopesha askari wake kote nchini, kwa lengo la kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na matamanio ya kujipatia fedha isivyo halali pamoja na rushwa.
Mkaguzi wa jeshi la polisi kutoka chama cha kuweka na kukopa makao Makuu ya Polisi Shabani Jumbe amesema askari wa Jeshi hilo bado wana nafasi kubwa ya kupaa kiuchumi kama watatumia vyema fursa zilizopo ndani ya jeshi
Askari kwa upande wao wamedai kuwa awali walikuwa na uelewa mdogo kuwa ndani ya Jeshi kuna taasisi zinazo weza kuwasaidia kutafuta fedha nje ya mfumo wa jeshi hilo
Aidha viongozi wa jeshi hilo Mkoani Arusha wamesema mwaka 2016 ni wakati wa kujiuliza walipokosea na kuanza ukurasa mpya ili kuepuka vitendo visivyo na maadili na kwamba askasri wanapaswa kujitathimini upya na kuangalia njia mbadala za kujikwamua kiuchumi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini