Kaimu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amesema
afya ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo imeimarika na leo ataruhusiwa.
Kardinali Pengo alifikishwa katika hospitali hiyo Desemba 31, mwaka jana kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Profesa Janabi alisema Pengo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo. Hata hivyo, hakueleza kwa undani.
Jana,
kwa mara ya kwanza tangu afikishwe katika hospitali hiyo, Pengo
alijitokeza hadharani na kuzungumza na wafanyakazi wa taasisi hiyo na
waandishi wa habari, huku akishukuru kwa huduma alizopata.
Alisema
amepatiwa huduma nzuri na kumfanya afute kichwani mwake habari za watu
mbalimbali wanaodai kuwa MNH haiwahudumii vizuri wagonjwa.
“Nataka
niwashukuru wahudumu wote walionifikisha katika hali hii, hasa Profesa
Janabi na Mkuu wa Kitengo cha Dharura na Ajali, Dk Juma Mfinanga,” alisema.
Akiwa
hospitalini hapo jana, Kardinali Pengo alitembelewa na maaskofu
wasaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Titus Mdoe na Eusebius Nzigilwa
pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea, Damian Dallu.
Kwa
upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na
Watoto, Ummy Mwalimu alisema Serikali imejipanga kuhakikisha wagonjwa wa
moyo hawapelekwi nje ya nchi kutibiwa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini